Hali ilivyokuwa nje ya Makao Makuu ya Kampuni ya Majembe Auction Mart jijini Dar.
Jengo la Majembe Auction Mart lililopo eneo la Mikocheni, Dar es Salaam.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya Makao Makuu ya Majembe Auction Mart , Dar.
Moja ya gari lililodaiwa kuwa wa Kampuni ya Yono Auction Mart likiwa limetolewa upepo kwenye matairi yote baada ya wahusika kutoweka eneo hilo.
Taswira ilivyokuwa eneo hilo.
Kampuni mbili zinazojishughulisha na udalali na kudai madeni nchini, Majembe Auction Mart na Yono Auction Mart zilijikuta zikivaana ana kwa ana Makao Makuu ya Majembe, Mikocheni B jijini Dar na wafanyakazi kusambaratika baada ya kuzuka mzozo uliosababisha polisi kufika na kuanza kupiga mabomu ya machozi baada ya pande mbili hizo kutoelewana, hakuna upande uliopatikana kuzungumzia mzozo huo.
Haikuweza kujulikana mara moja kiini cha sakata hilo, hata hivyo, Global TV ilibaki ikifuatilia. Kwa habari zaidi tembelea mtandao wetu huo wa Global TV ONLINE kujua zaidi.
NA DENIS MTIMA/GPL