×

Mabosi Simba Washtuka, Wamaliza Shoo Kimyakimya

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), Imani Kajula.

HUKU ikiwa inasubiriwa tarehe rasmi ya kufunguliwa kwa dirisha la kubwa usajili hapa nchini kwa ajili ya msimu ujao wa 2023/24, uongozi wa Simba umeshtukia jambo na kutamba kuwa sasa wanafanya mambo yao kimyakimya ili kuepuka vita za kugombea mchezaji.

Kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara 2023/24, Simba tayari wameanza kufanya maboresho ya kikosi chao ambapo wametangaza kuachana na winga wao wa kimataifa wa Ghana, Augustine Okrah.

Simba ambao wamemaliza msimu 2022/23 bila taji la mashindano rasmi, wanahusishwa na majina makubwa yakiwemo straika wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Ranga Chivaviro ambaye pia anatajwa kumalizana na Yanga, winga wa AS Vita, Erick Kabwe, Yahya Mbegu na Luis Miquissone.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema: “Kama timu tumesikitishwa sana baada ya kushindwa kufikia malengo ya msimu huu kama ambavyo ilikuwa msimu uliopita, hii inatufanya tujipange zaidi kwa msimu ujao. Tunajua kushinda ubingwa unahitaji wachezaji bora na timu imara.

“Tayari tumeanza kutafuta wachezaji sahihi na kutengeneza timu madhubuti kimya kimya ili kuepuka uwezekano wa kuvamiwa na timu ambazo mara zote zimekuwa zikituiga.”

STORI NA JOEL THOMAS

Leave a Comment