×

Nyota wa Senegal Yupo kwenye Hatihati Kukosekana Kombe la Dunia

Sadio Mane amepata majeruhi ya mguu

NYOTA wa Timu ya Taifa ya Senegal na klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani Sadio Mane yupo katika hatihati ya kukosekana kwenye fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka 2022.

 

Mane alipata majeruhi katika mchezo dhidi ya Werder Bremen baada ya kuumia mguu katika dakika ya 20 kwenye mchezo ambao klabu hiyo iliibuka na ushindi wa bao 6-1

Bayern Munich imeibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Werder Bremen

Zimebaki takribani siku 12 hadi kufunguliwa kwa mashindano ya Kombe la Dunia ambapo mchezo wa kwanza wa Senegal utakuwa ni dhidi ya Uholanzi.

 

Katika mchezo huo ambao Bayern Munich iliibuka na ushindi mnono, mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Jamal Musiala, Leon Goretzka, Tel pamoja na Serge Gnabry aliyefunga mabao matatu (3) Hat Trick.

Leave a Comment