
Chuo Kikuu Dodoma imehitimisha maonesho ya vyuo vikuu Nchini ambayo yaliandaliwa na TCU kwa mafaniko makubwa ya kutoa huduma ya Udahili kwa wanafunzi waliofika katika Viwanja vya Mnazi mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari Julai, 22,2023, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma,Mipango, fedha na utawala,Prof.Wineaster Andarson amesema ukubwa wa chuo ambacho ni kikubwa Tanzania na Afrika ya kati na uwezo wa kutoa wanafunzi Bora zaidi ndio Muhimbili mkubwa ambao umewafanya wanafunzi wengi mwaka huu kupata muitikio na kufanya Udahili kwa wingi.

“Chuo chetu kina toa wataalamu wengi na wenye ujuzi wa hali juu,hii ni kutokana na uwezo wa ufundishaji wa wakufunzi wetu ni wa hali ya juu,ni kwamba mwanafunzi ambaye amemaliza katika chuo chetu anaweza akaajiriwa Serikalini au kwenye sekta binafsi na pia huwa wanaajiriwa hapa hapa katika chuo chetu.
Hivyo basi niwakaribishe wanafunzi waendelee kufanya Udahili kupitia online platform yetu ya chuo,kwa kuwa elimu ambayo wataipa hapa ni kubwa ambayo akimaliza kusoma ataweza kupata ajira ndani ya Nchi na nje ya Nchi kwa sababu tunazalisha wafanyakazi wa Kimataifa,” amesema Prof. Andarson.
Kwa upande wa wanawake amewaasa kitumikia vyema nafasi wanazopewa ili kutoliangusha Taifa,kwa kuwa tunaongozwa na Raisi Jemedari ambaye ni Raisi wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan,hivyo basi ni vyema wakatimiza majukumu katika ubora wa hali ya juu.
“Tuendelee kujitahidi kujitahidi tukipewa nafasi tujue ni heshima ni dhamana kwa hiyo ili tisiwaangushe wale wanaotuteua lakini vile vile tusiiangushe Tanzania,wanawake Wana uwezo wa kufanya mambo mengi kwa wakati Mmoja.
Huduma muhimu ambazo zilizotolewa kwenye banda hilo kuwa ni udahili wa moja kwa
moja wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo hicho kwa Programu mbalimbali za masomo kwa
mwaka 2023/24, ushauri wa kitaalamu kuhusu programu, huduma za malazi, na masuala mengine
yanayohusu shughuli za Chuo Kikuu cha Dodoma.
Chuo Kikuuu Cha Dodoma kinatoa mafunzo katika fani za Udaktari, Uchumi, Sheria, Sosholojia,
Utawala wa Biashara, Biashara na Uhasibu, Biashara katika Utawala na Rasilimali Watu, ujasiriamali,
Biashara ya Kimataifa, Utalii, Masoko, Mazingira, Takwimu, Ununuzi na Ugavi, Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA), Jiolojia, Kemia, Madini, Petroli, Nishati Mbadala, Elimu, lugha, Uhusiano wa Kimataifa, ikolojia, Uandishi wa Habari na Mahusiano ya Umma, fizikia, na nyinginezo.
Zaidi ya Programu 80 katika ngazi ya Shahada za Awali zinatolewa na UDOM, na kwa ngazi ya Shahada za Umahili (Postgraduate Diploma, Masters & PhD) Programu zaidi ya 56.