×

Mshambuliaji Mpya Hafiz Konkoni Amkosha Gamondi Yanga

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Hafiz Konkoni.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Muargentina, Miguel Gamondi, amemuangalia mshambuliaji wake mpya, Hafiz Konkoni na kutamka kwamba, nyota huyo atakuwa tishio msimu wa 2023/24.

Konkoni amesajiliwa na Yanga kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Mayele ambaye amejiunga na Pyramids FC ya Misri, baada ya kuitimikia Yanga kwa kipindi cha misimu miwili.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema anaamini mshambuliaji huyo ataifanyia makubwa Yanga baada ya kuona kiwango chake mazoezini na katika michezo ya kirafiki ambayo wameicheza kambini kwao Kijiji cha Avic Town, Kigamboni, Dar es Salaam.

Gamondi alisema kuwa, anamtabiria mshambuliaji huyo kufanya vizuri zaidi ya Mayele baada ya kuona umahiri mkubwa wa kufunga na kutengeneza mabao kwa wachezaji wenzake.

Aliongeza kuwa, kikubwa mashabiki wampe ushirikiano mshambuliaji huyo akiwa anaipambania timu.

“Ninaamini mshambuliaji wangu mpya Konkoni atafanya vizuri zaidi ya mtangulizi wake Mayele, kitu kikubwa na chenye umuhimu ni mashabiki wa Yanga kumpa sapoti na kumjengea imani.

STORI NA WILBERT MOLANDI

KIVUMBI KINAANZA LEO NGAO ya JAMII/ MASTAA WAPYA WATAMBIANA/ KOCHA SIMBA ATUMA SALAMU…

Leave a Comment