×

Waziri Bashe: Bei Ya Vanilla Ya Tsh. Milioni 1.5 Kwa Kilo Haipo Duniani – Video

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

Waziri wa Kilimo ametoa jibu hilo wakati akizungumza kuhusu Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika utakofanyika Sept. 5-8, 2023
Bashe amesema “Bei ya Tsh. Milioni 1.5 kwa kilo ni uongo, nimesikia iliandikwa na Gazeti, ni vizuri kutochukua taarifa ambazo hazina uthibitisho. Kwahiyo bei ya Tsh. Milioni 1.5 kwa kilo haipo duniani, bei ya Tsh. Laki 5 kwa kilo haipo duniani”
Ameongeza kuwa “Tanzania tunazalisha Vanilla kwa kiwango kidogo. Vanilla ilipanda bei miaka miwili mitatu baada ya Madagascar kukumbwa na Vimbunga kwasababu wao ni Wazalishaji wakubwa, ikasaidia Wakulima wetu kupata bei nzuri”

Leave a Comment