×

Afrika Kusini: Wabunge Wapinga Trevor Noah Kulipwa Bilioni 4.2 Kutangaza Utalii

Mchekeshaji na mtangazaji maarufu nchini Marekani, Trevor Noah.

Pendekezo la kumlipa Mchekeshaji na mtangazaji maarufu nchini Marekani, Trevor Noah, Randi Milioni 33 (takriban Tsh. Bilioni 4.2) kwa Video ya Dakika 5 ya kuitangaza Afrika Kusini kama kivutio cha kitalii, limesababisha mpasuko baada ya baadhi ya Wabunge na Wananchi kupinga kwa kudai kuwa Nchi hiyo inapitia Mgogoro mkubwa wa kifedha kwa wakati huu.
Akitoa pendekezo hilo, Waziri wa Utalii, Patricia de Lille amesema kuwa Mchekeshaji na Mtangazaji huyo atalipwa na Baraza la Biashara la Utalii nchini humo, (Shirika Mwamvuli linalowakilisha Wadau wa Usafiri na Utalii wa Nchi hiyo) na sio kwa fedha za Umma

Hata hivyo, Wadau wengine wameunga mkono pendekezo hilo wakisema ushawishi wa Nyota huyo unaweza kukuza Utalii wa Afrika Kusini

KULA CHAKULA CHENYE SUMU – NINI UFANYE HALI HII INAKUPOTOKEA? | MAISHA na AFYA – VOA

Leave a Comment