
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua George Nathaniel Mandepo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Mandepo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usuluhishi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Bw. Mandepo anachukua nafasi ya Mhe. Griffin Venance Mwakapeje ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. George Daniel Yambesi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kwa kipindi cha pili.
