×

Waziri Ahukumiwa Kufanya Kazi Ngumu

ALIYEKUWA Waziri wa Afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Oly Ilunga, amehukumiwa kufanyishwa kazi ngumu kwa miaka mitano kwa kosa la kuiba Dola 400,000 (Sh. za Tanzania milioni 912) zilizotolewa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini humo.

 

Ilunga na mshauri wake wa masuala ya fedha walighushi stakabadhi kutoka kampuni feki kuhalalisha manunuzi. Sambamba na hukumu hiyo Ilunga amepewa masharti ya kutokuwa kiongozi wa umma tena.

 

Ilunga alikuwa waziri wa afya wa DRC kuanzia mwaka 2016 hadi mwezi Julai mwaka jana alipowekwa chini ya ulinzi.

Leave a Comment