×

Total Energies Yasherehekea Wiki Ya Huduma Kwa Wateja 2023 Kwa Kufungua Mlango Mpya Wa Huduma Bora

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd, Mamadou Ngom (wa pili kulia) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Hashim Abdallah Komba wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta kilichopo Kinyerezi Tabata wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Wa kwanza kulia ni Getrude Mpangile, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Masuala ya Mashirika, Rasilimali Watu na Utawala kutoka TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd.

Dar es salaam– 2nd October 2023 –Katika ijtihada za kukuza upatikanaji wa nishati yenye viwango vya juu na uhakika, kampuni Total Energies Marketing Tanzania wamezindua kituo kipya cha mafuta kilichopo Tabata Segerea ili kuwapa wateja wake huduma za uhakika popote walipo.

Uzinduzi huu umefanyika katika ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja, hafla  iliyohudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Ubungo, Mheshimiwa Hashim Komba aliemwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mtandao wa TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd Abdul Siddique akikagua gari la mteja wakati wa uzinduzi wa wiki ya utoaji huduma kwa wateja.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa kampuni hio, Mamadou Ngom alisema kuwa uzinduzi huo wa kituo kipya umezingatia mahitaji na maombi ya wateja wanaopatikana kitongoji cha Tabata Segerea na barabara ya Kinyerezi. Alinukuliwa, ‘wakati tunasheherekea wiki ya huduma kwa wateja, kampuni yetu inajivunia kufungua kituo hiki kipya kama sehemu ya ndoto yetu katika kuwapa nishati bora na safi kwa ajili ya vyombo vyao vya moto. Tunataka kuwaambia wote kuwa tunawasikiliza na tunahakikisha wanapata vitu vizuri wanavyostahili’.

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd, Mamadou Ngom akisafisha kioo cha gari la mteja wakati wa uzinduzi wa wiki ya utoaji huduma kwa wateja.

Aidha, Mhe Hashim Komba nae alisema, ‘uzinduzi huu wa kituo hiki ni hatua kubwa sana katika mkoa wetu hasa kwa wakazi wa Tabata Kinyerezi na watumiaji wa barabara zake. Hii ni ishara nzuri kwa wawekezaji wetu kuwa wako tayari na wanaendelea na kufungua fursa za ajira na pia hii itachangia ongezeko la sekta ya usafirishaji’.

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Ltd.

Kampuni ya Total Energies Marketing Tanzania imedhamiria kutoa huduma za mafuta kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wote popote walipo ili kukuza ufanisi katika sekta ya usafirishaji ila pia kuhakikisha ufanisi huo unawaletea manufaa zaidi katika kukuza uchumi wao kwa ujumla.

Leave a Comment