Magifti Dabodabo Ya Tigo Yazidi Kunogesha Msimu Wa Sikukuu, Yaanza Kumwaga Zawadi Mikoani
Global Publishers November 24, 2023 0 Comments
SHARE THIS:
Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo baada ya kuzindua kampeni ya Magifti Dabobado Jijini Dar ambayo inalenga kuwazawadia wateja wa Tigo, sasa imepiga hodi mikoani na kuanza kumwaga zawadi kwa washindi.
Katika kampeni ya Magifti Dabodabo kila atakayejishindia atamchagua na mpendwa wake naye kupata zawadi kama hiyo na hivyo kuwa magifti Dabodabo.
Mkurugenzi wa Tigo Zanzibar Aziz Ali (kushoto) akimpa Mkuu wa Wilaya ya Mjini (Znz), Rashid Simai Msaraka (katikati) zawadi ya fulana, wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Magifti Dabodabo iliyofanyika visiwani Zanzibar, Meneja wa tigo kanda ya Unguja Visiwani, Mwajuma Senkanga (kulia) akishuhudia.
Kampeni hii imebisha hodi mikoani ambapo wateja wa Mwanza, Mtwara na Zanzibar wameanza kunufaika na magifti hayo Dabodabo.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Joseph Mutalemwa (wa pili kushoto) akimpatia zawadi ya fulana mteja wa mtandao wa Tigo Alicia Benedicto, wakati wa uzinduni wa promosheni ya Magifti Dabodabo iliyofanyika jijini Mwanza, Meneja wa tigo kanda ya Ziwa Kaskazini Robert Sanyagi (kushoto) na Meneja Biashara Tigo Pesa Kanda ya Ziwa Christopher Charles wakishuhudia.