×

Mfungwa wa Marekani aliyekuwa gerezani kwa miaka 48 aondolewa mashtaka

Jaji wa Oklahoma amemuondolea mashtaka mtu ambaye alikuwa gerezani kwa karibu nusu karne kwa mauaji ya 1974, kifungo kirefu zaidi cha makosa kutumikia Marekani.

Glynn Simmons, 70, aliachiliwa mnamo Julai wakati hakimu alipoamuru kesi mpya isikilizwe.

Lakini wakili wa wilaya alisema siku ya Jumatatu hakukuwa na ushahidi wa kutosha kutoa idhini.

Katika agizo la Jumanne, Jaji wa Wilaya ya Oklahoma County Amy Palumbo alitangaza kuwa Bw Simmons hana hatia.

“Mahakama hii imepata ushahidi wa wazi na wa kuridhisha kwamba kosa ambalo lilimtia hatiani Simmons, kuhukumiwa na kufungwa… halikufanywa na Simmons,” alisema katika uamuzi wake.

Glynn Simmons anasema muda wake gerezani ni “funzo la uvumilivu na ukakamavu maishani”

SHILOLE AMWAGA MACHOZI AKIJIZAWADIA GARI LA MIL 70 KWENYE BIRTHDAY YAKE – AKATA MAUNO…

Leave a Comment