Polisi anayefahamika kwa jina la Sweet Thadeo, ambaye kituo chake cha kazi ni Usa-River Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha anadaiwa kufanya majaribio ya kumuua mume wake kwa kumtumia majambazi kufanya tukio hilo.
Inaelezwa hapo awali alikodi majambazi kutoka Dar es Salaam wanao tumia silaha za moto lakini walishindwana kwenye bei na tukio hilo kushindwa kukamilika, hivyo alijaribu tena kukodi majambazi kutoka Arusha wanaotumia silaha za jadi kwa makubaliano ya shilingi milioni 3 na ilipofika Desemba 26, 2023 majambazi hao walifanya tukio hilo getini nyumbani kwake alipokua akirudi nyumbani.