×

Baraza La Uuguzi Na Ukunga Lafuta Matokeo Ya Mtihani Wa Usajili Na Leseni Kwa Watahiniwa 1,330 Wa Stashahada

Taarifa ya Wizara ya Afya imeeleza kuwa Mnamo Septemba 7, 2023, Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania liliendesha Mitihani ya Usajili na Leseni kwa Wauguzi na Wakunga 1,434 wa ngazi zote (Astashahada 44, Stashahada 1,330 na Shahada 60) katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza pamoja na Dodoma

Baada ya kupata taarifa, Wizara ya Afya ilithibitisha kuwa Mtihani ulivuja na kusambaa kwa Watahiniwa wa Stashahada hali iliyosababisha matokeo kufutwa. Mtuhumiwa aliyehusika katika uvujishaji wa Mtihani huu tayari amesimamishwa kazi huku taratibu za Kinidhamu na Kisheria zikiendelea

Taarifa hiyo imeeleza zaidi kuwa Watahiniwa watapewa nafasi ya kufanya Mtihani mwingine Februari 16, 2024 bila malipo yoyote na hawatahitajika kujisajili tena ambapo Mtihani utafanyika Dodoma

 

Leave a Comment