×

Barcelona na Arsenal Watinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

Klabu ya Barcelona na Arsenal wametinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Arsenal wakitinga kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 kufuatia ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya FC Porto.

Dakika 90 zilimalizika Arsenal wakiwa mbele 1-0 ikiwa ni sare ya jumla ya 1-1 kufuatia kipigo cha 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza.

Muda wa ziada haukuzaa goli hali iliyopelekea mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Pia Barcelona imetinga hatua hiyo kufuatia ushindi wa jumla wa 4-2 dhidi ya Napoli kwenye hatua ya 16 bora.

Barcelona imetinga robo fainali kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2019/20.

#EXCLUSIVE: MKUBWA FELLA AFUNGUKA ZUCHU KUFUNGIWA ZANZIBAR – ”HAKUTUKANA – MASHABIKI WAMETUKANA”

Leave a Comment