
Shughuli ya kuhesabu kura nchini Afrika Kusini inaendelea, ambapo kwa mujibu wa matokeo baada ya takriban asilimia 90 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa Jumatano zimehesabiwa kufikia Ijumaa, Mei 31, 2024 Chama tawala ANC kinaelekea kupoteza wingi wa viti bungeni
Afrika Kusini huenda ikaunda serikali ya mseto kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kufuatia uchaguzi wa bunge uliofanyika nchini humo. Hii ni kulingana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEC).
