Dar es Salaam, Juni 14, 2024: Bolt, Kampuni inayoongoza kwa huduma za usafirishaji Tanzania na Barani Afrika, imezindua kituo cha huduma kwa madereva katika juhudi zake za kuimarisha uhusiano wa madereva na kutimiza matarajio ya madereva kwa kushughulikia matatizo yao.
Kituo cha huduma kwa madereva kiko katika Jengo la 395 Ursino, Makutano ya Morocco, Barabara ya Mwai Kibaki na kitakuwa kinatoa huduma kwa mfumo miadi ili kuhakikisha usimamizi wa masuala ya madereva unakuwa wa ufanisi na bila vikwazo.

Uzinduzi wa kituo hicho kitasaidia kuongeza utoaji wa faida mbalimbali, ikiwa ni pamoja na usaidizi bora wa madereva, njia bora za mawasiliano, fursa za mafunzo, kujenga jamii, utatuzi wa masuala, kuthamini madereva, na kuwa na muonekano wa chanya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho, Dimmy Kanyankole, Meneja Mkazi wa Bolt Tanzania alisema: “Wabia wetu madereva ndio msingi wa biashara yetu, hivyo, Bolt imejipanga kuhakikisha mahitaji yao yanashughulikiwa na kutatuliwa kwa ufanisi na kwa wakati.
Kuzinduliwa kwa kituo hiki kipya ni uthibitisho kwamba tumejitolea kuimarisha ustawi wa madereva wetu na ushirikiano, ambayo hatimaye utachangia mafanikio na ukuaji wa biashara yetu na sekta ya usafiri kwa ujumla. Tutaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau wetu wote muhimu ili kuendelea kutoa huduma za gharama nafuu, salama na huduma zinazofaa za usafiri wa kukodi mtandaoni nchini Tanzania; pia kutengeneza fursa za ujasiriamali zinazowezesha watu wengi zaidi kujipatia kipato endelevu.”
Bolt inaendelea kufanyia kazi uzoefu wa madereva kila mara, na kutoa msaada wanaohitaji ili kufanikiwa katika biashara zao. Kampuni pia inaendelea kuchambua na kuvumbua huduma zake kwa manufaa ya madereva na abiria wake