
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari Temeke, Joseph Mafuru (15) ameuawa na watu wanaotajwa kuwa vibaka wakati wakitaka kumpora simu.
Tukio limetokea majira ya saa moja, usiku wa Juni 18, 2024 katika eneo la Temeke Mikoroshini, Kata ya Sandali jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Joseph alitumwa kumpelekea chakula baba yake ambapo wakati anarudi nyumbani, ndipo alipokutana na vibaka waliotaka kumpora simu na katika majibizano, ndipo walipomchoma kwa visu na bisibisi na kusababisha mauti yake.