×

Simba Kuanza Shirikisho kati ya Uhamiaji au Bingwa wa FA ya Libya

Klabu ya Simba itakutana na mmoja kati ya Uhamiaji ya Zanzibar au Bingwa wa FA ya Libya, Libya 1 kwenye raundi ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2024/25.

Timu ya Uhamiaji ya visiwani Zanzibar imepangwa dhidi ya wawakilishi hao kutoka Libya katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali CAFCC ambapo mshindi wa matokeo ya jumla atakutana na Mnyama kwenye raundi ya kwanza.

Wanamangush, Coastal Union watakabiliana na FC Bravos ya Angola kwenye hatua ya awali ambapo mshindi wa matokeo ya jumla atachuana na Fc Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Leave a Comment