
Inspekta Jenerali wa polisi nchini Kenya, Japheth Koome leo Julai 12, 2024 amejiuzulu kufuatia wiki kadhaa za maandamano ambapo zaidi ya watu 40 waliuawa.
Mashirika ya haki za binadamu yameshutumu polisi kwa kuwapiga risasi makumi ya waandamanaji baadhi yao kuwaua na kuwateka nyara au kuwakamata kiholela.
Maandamano yalizuka nchini Kenya katikati ya mwezi uliopita kupinga mapendekezo ya nyongeza ya ushuru. Waandamanaji walivamia bunge muda mfupi baada ya wabunge kupitisha mswada huo.