×

Hitilifu ya Teknolojia Yasimamisha Dunia, Mashirika ya Ndege, Mabenki Yashindwa kutoa huduma

Hitilafu kubwa ya kiteknolojia iliyotokea asubuhi ya leo Ijumaa, Julai 19, 2024 imesababisha mashirika makubwa ya ndege duniani kusitisha safari zao, mabenki kushindwa kutoa huduma kwa wateja, vyombo vya habari vya kimataifa kushindwa kurusha matangazo yao pamoja na kusimama kwa huduma nyingine nyingi zinazoendeshwa kwa kutumia teknolojia.

Hitilafu hiyo imesababishwa na matatizo ya kiufundi yaliyoikumba Kampuni ya Microsoft kupitia huduma yake ya Microsoft Cloud Computing ambayo inatumiwa na karibu mashirika yote makubwa duniani kuendesha huduma na biashara zao.

Inaelezwa kuwa hitilafu katika huduma hiyo ya Microsoft, imezilenga zaidi kompyuta zinazotumia mfumo wa uendeshaji wa Windows ambapo mamilioni ya kompyuta zinazotumia mfumo huo, zilijizima na kuonesha screen ya bluu.

Mashirika ya ndege kama American Airlines, Delta Airlines na United Airlines nchini Marekani, yote ametoa taarifa ya ndege zao zote kutua kwa dharura huku abiria wengi wakilazimika kusubiri kwenye viwanja vya ndege, wakiwa hawajui hatma yao.

Nchini Australia, uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa, Sydney Airport uliwatangazia abiria wote kwamba kutakuwa na kuchelewa kwa huduma za usafiri kutokana na tatizo hilo.
Barani Ulaya, Uwanja wa Ndege wa Brandenburg jijini Berlin, nao umetoa taarifa za kusitishwa kwa huduma zake zote huku nchini Hispania, viwanja 46 vya ndege navyo vimesitisha huduma zake kutokana na tatizo hilo.

Treni za mwendokasi nchini Uingereza, nazo zimeathiriwa na tatizo hilo na kusababisha huduma zote zisitishwe.

YANGA WATUA AFRIKA KUSINI KIBABE -WAPO TAYARI KUKIPIGA na FC AUSBURG ya UJERUMANI na KAIZER CHIEFS..

Leave a Comment