
Familia ya mtoto Maliki Hashimu (6) mkazi wa Goba jijini Dar, ambaye wiki moja iliyopita inadaiwa alifanyiwa kitendo cha kikatili na dada wa kazi wa nyumbani kwao aliyefahamika kwa jina la Clemensia Cosmas baada ya kumkata shingoni na kitu cha ncha kali mpaka kutenganisha koromea na njia ya hewa, wazazi wa mtoto huyo wameibuka na kusema wamemsamehe kutoka hausigeli huyo.
Wakizungumza na Global TV, wazazi hao ambao kwanza walitoa shukrani kwa Rais kwa kugharamia matibabu yote ya mtoto huyo na Jeshi la Polisi kwa jitihada zao, wamesema wanaiachia serikali jambo hilo na kusisitiza kwamba wao wamemsamehe kwa moyo mmoja.