×

Mtanzania Akwama India, Afungiwa Kambini, Bila Mil 3 Hawezi Kurudi, Mama’ake Aomba Msaada – Video

Mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma Bakary, mkazi wa Mwandege, Mkoani Pwani ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iweze kumsaidia mtoto wake, ambaye amefungiwa kwenye kambi maalumu huko nchini India, baada ya kupitiliza muda wa kuishi nchini humo bila kibali.

Akizungumza na Global TV kwa uchungu mama huyo alisema kuwa mtoto wake takribani miaka 7, aliondoka na kumuachia mtoto mdogo wa chekechea na mpaka sasa hivi mtoto huyo yuko Darasa la Sita, alafu yeye kwa sasa anaumwa sana kutokana na kufanyiwa upasuaji wa tumbo mara mbili.

“Natamani mtoto wangu arudi hata aje anasaidie jamani nataseka na mtoto wake aliteniachia amechukuliwa na mwalimu ili kuweza kunisaidia maana maisha yangu yote nilikuwa namtegemea yeye” alisema mama huyo.

Leave a Comment