
Afisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa mtandao wa YouTube na mmoja wa wafanyakazi wa kwanza wa Google, Susan Wojcicki amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 56 baada ya kusumbuliwa na tatizo la satarani kwa kipindi cha miaka miwili.
Akitangaza taarifa ya kifo hicho siku ya Ijumaa Mume wake, Dennis Troper kupitia chapisho lake kwenye Facebook alisema: “Ni kwa huzuni kubwa kwamba ninashiriki habari za kifo cha Susan Wojcicki. Mke wangu mpendwa wa miaka 26 na mama wa watoto wetu watano walituacha leo baada ya miaka miwili ya kuishi na saratani ya mapafu”