×

Waliomuua Kinyama Milembe Wa Geita Wahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa – Video

Washitakiwa Watatu kati ya wanne walioshtakiwa kwa kosa la mauaji ya Milembe Suleiman (43), wametiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa leo Jumanne Agosti 21, 2024 Hukumu iliyosomwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Geita, Kelvin Mhina.

Mahakama imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ambao umethibitisha kosa hilo pasipo kuwa na shaka.

Jaji Mhina aliyesikiliza kesi hiyo amesema kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri, Mahakama imewatia hatiani washtakiwa wa kwanza hadi wa tatu na kumuachia huru wa nne, Musa Lubingo.

Washitakiwa Waliotiwa hatiani katika kesi hiyo ya jinai namba 39 ya mwaka 2023 ni mshtakiwa wa kwanza, Dayfath Maunga (30), wa pili ni Safari Lubingo (54), na wa tatu ni Genja Pastory.

Leave a Comment