Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawataarifu Walipakodi na wananchi kwa jumla kuwa, Ofisi za TRA nchi nzima zitakuwa wazi kuwahudumia walipakodi siku ya Jumamosi ya Agosti 31, 2024 kuanzia saa 2:30 Asubuhi mpaka saa 11:00 jioni.
Hatua hii inatokana na ushauri na maoni ya wadau wa kodi, hivyo TRA inawakaribisha walipakodi wote kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali za kikodi.
