×

Polisi Wamjibu Mbowe, Wapiga ‘Stop’ Maandamano ‘Wasithubutu Kuandamana’- Video

Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania DCP David A. Misime

MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime leo Septemba 13, 2024 amesema Jeshi hilo limepiga marufuku Maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA yaliyoitishwa Septemba 23 mwaka huu.

“Kutokana na taarifa hiyo, Jeshi la Polisi nchini linatoa onyo kwa viongozi wa chama hicho kuacha kuendelea kuhamasisha wananchi kujihusisha katika uhalifu huo na yeyote atakayeingia barabarani atakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za nchi, kwa maana hiyo maandamano hayo yamepigwa marufuku, jeshi la polisi linatoa katazo kwa yeyote aliyealikwa, kuelekezwa kufika Dar es Salaam kutoka mkoa wowote ule kwa ajili ya maandamano hayo asithubutu kufanya hivyo kwani maandamano hayo ni haramu na hayatafanyika”- Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania DCP David A. Misime akizungumza na wanahabari Mjini Moshi.

Leave a Comment