
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo Septemba 13, 2024 amesema chama hicho hakikubaliani na matendo ya utekaji na mauwaji, na kwamba watu wanaofanya hivyo ni magenge yenye nia mbaya dhidi ya CCM
Akizungumza na Wahariri na Waandishi waaandamizi wa habari kwenye ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho, Lumumba jijjini Dar es Salaam leo, Ijumaa Septemba 13.2024 Balozi Dkt. Nchimbi amesema CCM katu haiwezi kuunga mkono matendo ya uhalifu kama hayo kwa kuwa yanaenda kinyume na miongozo na ilani ya chama hicho
Amesema chama hicho tawala hapa nchini kinaamini kuwa ongezeko la matukio ya aina hiyo kunasababisha mazingira magumu ya chama hicho kwa wananchi na kwamba umma unapaswa kupuuza wale wote wanaoamini wahalifu hususani wanaoendesha matendo ya utekaji na mauwaji ya kwamba wanaungwa mkono na CCM