The House of Favourite Newspapers

Mbunge amrejesha Zerish Bongo Muvi

0

Mayasa Mariwata

MBUNGE wa Morogoro Kusini, Prosper Mbena amemrejesha kwenye ulingo mkongwe wa filamu Bongo, Hellen Luanda ‘Zerish’ baada ya kukaa kimya kwa kipindi kirefu.
Akizungumza na Showbiz Xtra Zerish aliyewahi kubamba na Filamu ya Niite Mama akiwa na King Majuto alisema kuwa, kuna mambo mengi yaliyomfanya apotee kwenye sanaa yakiwemo masuala ya mapenzi lakini anamshukuru mbunge huyo ambaye ameshikilia bango kuhakikisha anamrudisha kwenye sanaa.
“Nilikaa kimya kwa kipindi kirefu sababu nilikuwa na mtu ambaye hakupenda nijihusishe na mambo ya sanaa, namshukuru huyu mbunge kwa kunirudisha upya na ameniahidi kunidhamini kwa kila kitu kwenye sanaa,” alisema Zerish.

Leave A Reply