×

Yanga Princess Hawatanii Wanataka Kombe

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa malengo makubwa ni kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwa Wanawake baada ya kufanikisha hesabu za kuivua ubingwa Simba Queens kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali.

Ipo wazi kwamba Simba walikuwa wanatetea taji hilo kwa sasa watapambana kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Ceasiaa Queens huku Yanga Princess ikikutana na JKT Queens iliyoshinda mabao 7-0 Ceasiaa Queens.

Mabao ya JKT Queens kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa mapema Oktoba 2 2024 Uwanja wa KMC, Mwenge na kuhudhuriwa na mashabiki wengi yalifungwa na Winfrida Gerald, Anastazia Katunzi, Stumai Abdallah, Stumai Abdallah, Stumai Abdallah na Janeth Matulanga.

Kwenye Kariakoo Dabi baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba Queens 1-1 Yanga Princess na kwenye changamoto ya penalti ilikuwa Simba Queens 3-4 Yanga Princess ambayo inanolewa na Kocha Mkuu Edna Lema.
Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua umuhimu wa ushindi kwenye mchezo wao wa Dabi ya Wanawake hesabu zao kubwa ni kutwaa taji hilo la Ngao ya Jamii.

“Tunatambua ushindani ni mkubwa na walijipanga wapinzani wetu kushinda mwisho tumepata matokeo na sasa ni kazi kuelekea kwenye mchezo wetu wa fainali tunatambua utakuwa na ugumu lakini tupo tayari kwa mchezo huo mashabiki wajitokeze kwa wingi.”

KAMANDA MULIRO – “TUMEWAKAMATA WALIOTEKETEZA LORI NA KUIBA MADINI YA KOPA”..

Leave a Comment