Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda Novemba 3, 2024 aliwasili nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Musuguri wilayani Butiama Mkoani Mara kwa ajili ya kutoa salamu za pole kwa wafiwa na kukagua maandalizi ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika leo.
Jenerali Mkunda amewashukuru wananchi wa Butiama na maeneo ya karibu kwa kushiriki katika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu ikiwa ni heshima kwa kiongozi huyo aliyetoa mchango mkubwa katika Ulinzi wa taifa letu.
Jenerali Musuguri alifariki Oktoba 29, 2024 akiwa na umri wa Miaka 104 na anatarajiwa kuzikwa kwa heshima zote za kijeshi.
