
Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Hemed Suleiman ametangaza majina ya wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya mwisho ya kufuzu michuano ya AFCON 2025 dhidi ya Timu ya Taifa ya Ethiopia na Timu ya Taifa ya Guinea.
Katika kikosi hicho, mshambuliaji wa Klabu ya Al-Talaba ya Iraq, Simon Msuva ambaye pia ni moja kati ya mchezaji mwenye uzoefu mkubwa akiichezea Taifa Stars zaidi ya michezo 90 amerejeshwa kikosini ili kuongeza nguvu kuelekea michezo hiyo muhimu ya kundi H.
Pia kocha Suleiman amewaongeza kikosini golikipa wa Simba, Aishi Manula na beki Shomari Kapombe waliokosekana katika kikosi hicho katika michezo ya hivi karibuni, huku mshambuliaji na nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Samatta naye akiendelea kujumuishwa katika kikosi hicho.
