×

Tetesi za Soka Ulaya July 05 2020

Inter Milan imeanza mazungumzo na Chelsea ya kumnunua beki wa kushoto wa Italia Emerson Palmieri, 25, kutoka klabu ya Stamford Bridge.

 

Chelsea imeanza tena mazungumzo kuhusu makubaliano mapya na mshambuliaji wa Brazil Willian, ambaye amehusishwa na Arsenal na Tottenham baada ya mchezaji huyo, 31, kukataa ombi la kuhamia klabu ambayo haikutajwa huko China.

Real Madrid inataka kumuuza mchezaji wa Colombia, James Rodriguez, 28, ambaye amesalia na mwaka mmoja kumaliza kandarasi yake badala ya kumpoteza mwaka ujao. Arsenal, Everton, Manchester United na Wolves inasemekana kwamba klabu zote hizo zimeonesha nia ya kutaka kumsajali.

West Ham imeungana na Everton, Manchester United na Southampton katika kuonesha nia ya kumwinda mlinzi wa Real Valladolid na Ghana Mohammed Salisu, 21.

Leave a Comment