Dar es Salaam, 13 Desemba 2024: Watumiaji wa mtandao wa simu wa Yas kupitia Kampeni yake inayoendelea ya Magift ya Kugift droo ya tano washindi watatu wamejinyakulia shilingi milioni moja kila mmoja.
Washindi hao walikabidhiwa hundi ya fedha walizojishindia na msemaji wa kampeni hiyo, Haji Manara maarufu kama Bugati.
Baada ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao Bugati aliwataka watumiaji wengine wa simu kutumia mtandao wa Yas kwa ajili ya huduma mbalimbali kama vile kufanya miamala mbalimbali kama vile kuweka na kutoa pesa, kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia Mixx By Yas zamani Tigo Pesa.Ameendelea kusema kuwa kwa kufanya hivyo unakuwa umeingia kwenye droo hiyo na hivyo kuweza kuondoka na zawadi mbalimbali kama vile simu janja, pesa taslimu shilingi milioni moja au kumi na kufurahia vyema kipindi hiki cha sikuu za Krismas na Mwaka mpya.