
JUMLA ya Wanafunzi 974,332 wakiwemo Wasichana 525,225 na Wavulana 449,107 ikijumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum 3,067 ambapo wasichana 1,402 na Wavulana 1,665 wamechaguliwa na kupangwa katika shule za Sekondari za Serikali kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2025 .
Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 16, 2024 jijini Dar es salaam, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2025
BONYEZA HAPA>>>WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA – 2025
Waziri Mchengerwa amesema kuwa uchaguzi wa Wanafunzi kujiunga Kidato cha kwanza mwaka 2025 umezingatia kigezo cha ufaulu wa Mtahiniwa anayechaguliwa ambapo kila mtahiniwa aliyefanya Mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mwaka 2024 na kupata jumla ya alama za ufaulu kati 121 hadi 300 amechaguliwa kujiunga na kupangiwa shule ya sekondari ya Serikali.

“Pia ninaomba nimeseme kuwa wanafunzi wote wenye sifa ya kujiunga kidato kwanza watapata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza bila ya kuwepo chaguo la pili kama iliyokuwa hapo awali hivyo wale wote waliopata ufaulu mzuri watajiunga kidato cha kwanza 2025”Amesema Mchengerwa
Aidha amesema kuwa shule za Sekondari za Serikali walizopangiwa wanafunzi zipo katika makundi mawili,shule za Bweni na shule za kutwa.
Aidha ameongeza kuwa katika shule za sekondari za bweni zimegawanyika katika makundi matatu ambayo,shule ya sekondari bweni za wanafunzi wenye ufaulu wa juu (Special Schools)shule za Amali za kihandishi (ufundi) na bweni taifa.
Waziri Mchengerwa pia amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2025 nchini watumie vizuri fursa waliyoipata kusoma kwa bidii ili wafikie malengo waliojiwekea na matarajio ya wazazi.