
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, leo amefanya mahojiano na Kipindi cha Frontpage cha Global Radio na Global TV moja kwa moja kutoka nyumbani kwake, Tegeta jijini Dar es Salaam.
Lissu amefunguka mengi na miongoni mwa aliyoyasema, ni kwamba Chadema ni chama chao wote, wapo waliojitolea mpaka uhai wao kwa hiyo watu wasibabaishane kwa kueleza kwamba mchango wa baadhi ya watu ni mkubwa kuliko wengine.
Pia ameeleza kuwa Sheria ya vyama vya siasa inaeleza kuwa, uongozi wa vyama vya siasa utapatikana na njia ya uchaguzi wa Kidemokrasia wa mara kwa mara
