×

HopeSprout Watoa Msaada katika cha Zaidia Orphanage cha jijini Dar

Shirika la HopeSprout ambalo linajishughulisha na kutoa misaada kwa Makundi Mbalimbali ya wasiojiweza kupitia mpango wake unaolenga katika elimu, huduma za afya, na maendeleo ya jamii umeweza kujumuika na Wototo wasiojiweza katika kituo cha Zaidia Orphanage cha jijini Dar es Salaam Kuandaa Mazingira Kuelekea katika sikukuu ya christmass na kutoa Msaada wa Mahitaji Muhimu katika kituo kicho.

Akizungumza Mwanafamilia wa Shirika hilo Bi Sumta Godfrey Amesema lengo la kujumuika na watoto hao kuwapa furaha kwenye sikukuu hii krismasi kama ambavyo watoto wamajumbani husherekea na hao watoto wanafasi hiyo pia.

HopeSprout inashirikiana na washirika wa ndani na washikadau ili kuhakikisha kwamba mipango yake ni nyeti kitamaduni, yenye athari, na inawiana na matarajio ya watu inayowahudumia.

“Dhamira yetu ni kutoa zana na usaidizi unaohitajika ili kuleta mabadiliko ya kudumu,” afisa wa HopeSprout alisema. “Tunaamini kuwa kila jumuiya ina uwezo wa kustawi inapopewa fursa zinazofaa

 

 

Leave a Comment