×

Mambo ni Moto! Paula Afunguka Mazito Siku ya Kuzaliwa Marioo


Sosholaiti maarufu kutoka Tanzania, Paula Kajala na mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva, Marioo  wameonyesha mapenzi yao wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Marioo hivi karibuni.

Katika ujumbe wa mahaba alioandika kwenye mitandao wa kijamii, Paula alimtakia mpenzi wake heri ya siku ya kuzaliwa kwa maneno yenye hisia kali:

“Happy birthday my love, my best friend, my partner, na baba watoto wangu. Umekuwa baba bora kwa mtoto wetu na mshirika mzuri katika safari yetu ya maisha. Wewe ni kila kitu kwangu, na nakupenda sana. Mungu akubariki kila unachoshika kikafanikiwe”

Mapenzi yao yanaendelea kuwa gumzo mitandaoni, wakivutia mashabiki na kuwapa matumaini ya uhusiano thabiti.

Leave a Comment