Godbless Lema aliyekuwa wakala wa Tundu Lissu kwenye uchaguzi wa uenyekiti ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema amepitia wakati mgumu sana kumpambania Lissu mpaka alipofanikiwa kushinda.
Lema akizungumza nje ya Ukumbi wa Mlimani City baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika, amesema haikuwa kazi nyepesi kuachana na Freeman Mbowe ambaye kwake ni kama kaka, na kumuunga mkono Lissu.