×

Breaking: Mbowe Ampongeza Lissu Kwa Ushindi, Mwenyekiti Mpya Chadema – Video

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa X, Freeman Mbowe amempongeza Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa na wanachama wa Chadema.

Mbowe ameandika:

“Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa mkutano mkuu wa chama chetu Chadema uliohitimishwa leo asubuhi, Januari 22, 2025.

Nampongeza mheshimiwa Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la uongozi wa chama. Nawatakia kila la heri katika kukipeleka mbele chama chetu.

Mbowe ameandika ujumbe huo wakati wanachama wa chama hicho wakiwa na shauku kubwa ya kusikia matokeo rasmi ya kinyang’anyiro cha uchaguzi huo.

Fuatilia matangazo mubashara ya kila kinachoendelea Mlimani City jijini Dar es Salaam kupitia Youtube, Global TV.

Leave a Comment