×

Brazil Yatoa Mafunzo Ya Usalama Kwa Vyombo Vya Usalama Tanzania

Brazil imetoa mafunzo maalum ya kukabiliana na uhalifu katika mikusanyiko mikubwa, viwanja vya michezo, Viwanja vya ndege, sehemu za mikusanyiko ya utalii, ulinzi wa watalii, Kuingia na kutoka kwa wageni nchini, usalama wa fukwe, na namna ya kuzuia majanga ya kuzama maji na moto.

Mafunzo hayo yalifanyika kuanzia Februari 20 hadi 21, 2025 yalifunguliwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Maduhu na washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kutoka Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji.

Mafunzo hayo yalifungwa rasmi Februari 21, 2025 na Balozi Kaganda anayeshughulikia mashirika ya kimataifa (Multilateral) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kupitia mafunzo hayo, Vyombo vya UsalamaTanzania vimejengewa uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuendelea kushirikiana na Brazili ambayo ni nchi inayoongoza kwa utalii duniani ikifuatiwa na Tanzania.