×

Watu 18 Wafariki Dunia, 32 Wajeruhiwa Katika Ajali Ya Basi Thailand

Watu 18 wamefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka kwenye mteremko wa barabara katika mkoa wa Prachin Buri, Thailand, leo Jumatano, Februari 26, 2025.

Gari hilo, ambalo lilikuwa limebeba abiria 49, lilipinduka saa 3:20 asubuhi kwa saa za ndani (saa 2000 GMT Jumanne).

Watu kumi na saba waliripotiwa kufariki papo hapo, huku mmoja akifariki hospitalini. Basi hilo lilikuwa moja kati ya mabasi matatu yaliyokuwa yakisafirisha watu 200 kutoka mkoa wa Bueng Kan, kando ya Mto Mekong, kuelekea Rayong.

Uchunguzi wa awali umeonyesha basi hilo la ghorofa mbili lilipata hitilafu ya breki na kupata ajali kwenye mteremko.
Waziri Mkuu wa Thailand, Paetongtarn Shinawatra, ametoa salamu za pole kwa familia za marehemu.