×

Doto Biteko Afanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje ya Misri

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Wamisri Waishio Nje wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Dkt. Badr Abdelatty jijini Dar es Salaam Machi 19, 2025.

Mazungumzo ya viongozi hao yameangazia ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi uliopo kati ya Tanzania na Misri.

Aidha, kwa upande wa sekta ya nishati wamezungumzia maendeleo ya mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere pamoja na ziara ya Mhe. Abdelatty wilayani Rufiji kutembelea mradi huo hapo kesho tarehe 19 Machi, 2025.

Tanzania na Misri zinaendelea kuboresha ushirikiano wa uwili katika sekta mbalimbali za kimkakati ikiwemo sekta ya nishati, viwanda, biashara, uwekezaji, ujenzi wa miundombinu, uchukuzi na elimu.