×

Ajenda ya Kidigitali Yashika Kasi Nchini Kupitia Future Ready Summit na Innovation Week 2025

Taifa la Leo! Vijana pia wakijadili changamoto na fursa zinazopatikana kupitia ubunifu, na namna wanavyoweza kuingia kwenye ulimwengu wa kidijitali na kujiajiri kwa kutumia suluhisho bunifu.
Fursa ya kipekee kwa vijana! Viongozi wa Rasilimali Watu kutoka katika mashirika na makampuni mbalimbali nchini Tanzania walikutana ana kwa ana na vijana walioko vyuoni bila kuwasahau wahitimu wa vyuo mbalimbali na kuwapa mbinu za kutafuta ajira, kuandika CV na jinsi ya kung’ara katika soko la ajira la sasa
Baada ya wasilisho lake kuhusu matumizi sahihi na salama ya Akili Mnemba (AI), Mo Gawdat (kulia), gwiji wa kimataifa katika masuala ya AI, alipata fursa ya kuonesha baadhi ya vitabu vyake kwa washiriki katika mkutano huo. Pichani ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah (kushoto) na Philip Basiimire, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Ubunifu kwa Vitendo! Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Patrobas Katambi akiangalia drone ambayo inawasaidia wakulima mkoani Morogoro kufanya kilimo cha kisasa zaidi kwa kutumia teknolojia ya kidijitali na hivyo kuongeza mapato yao.
Usalama wa kidijitali ni msingi wa maendeleo. Athumani Mlinga, Mkurugenzi wa TEHAMA wa Vodacom Tanzania, akizungumza na vijana wabunifu wakati wa zoezi mbashara la kufanya udukuzi salama katika mada ya ‘Ethical Hacking’

Ubunifu katika Misitu! Rais wa Finland, Alexander Stubb, akizindua mpango wa Green Catalyst unaolenga kuhamasisha ubunifu katika sekta ya misitu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania chini ya mradi wa ubunifu wa FUNGUO