
Dar es Salaam, 30 Juni 2025: Benki ya NMB imewakaribisha Wananchi wote kukaribia katika tawi lao lililopo Viwanja vya Maonesho vya Julius Nyerere kupata huduma zote za kibenki.
Akizungumza na wanahabari katika Viwanja hivyo, Mkuu wa Matawi na Mauzo NMB, Donatus Richard amesema kuwa anawajulisha Watanzania wote na wafanyabiashara kuwa tawi hilo ni benki kama yalivyo matawi yao mengine yaliyopo hapa nchini;
“Katika tawi hili huduma zote za kibenki zinatolewa ikiwemo kuweka pesa, kutoa pesa, kutoa Elimu sahihi ya kifedha, kupewa elimu namna ya kuhamisha fedha kulipa bili, kuingiza salio kupitia App ya NMB mkononi na huduma, mbalimbali zitolewazo na benki yetu amesema.
“Pia tumeboresha sana huduma zetu za NMB mkononi, huduma za bima, mikopo tunatoa mkopo wa kilimo biashara kwa njia ya kawaida na kimtandao, tunafungua akaunti ya mtoto hadi aliyezaliwa leo, hivyo basi hapa huduma zote watapata kupitia watoa huduma wetu.
“NMB inatarajia kuhudumia zaidi ya wafanyabiashara 3,000 na kupokea wateja zaidi ya 900,000 katika kipindi chote cha maonesho ya sabasaba mwaka huu hivyo tunatoa taarifa kuwa wale wafanyabiashara ambao bado hawana akaunti, huu ni wakati sahihi, tupo hapa kwa ajili yao.
“Pia tumeweka dirisha maalum kwa ajili ya ulipaji wa ada na kodi mbalimbali za serikali kama vile malipo ya vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA ) na mengineyo,” amesema Donatus na kuwakaribisha wote kwenda kwenye banda lao hilo lililopo katika maonesho haya ya Kimataifa ya 49 kujionea huduma ambazo wameziboresha ili mteja aweze kupata kilicho bora kupitia benki hiyo.