
Mjasiriamali mwanadada maarufu, Luiza Mosha, ametoa angalizo kwa jamii kuhusu umakini katika kushiriki siri binafsi na marafiki. Akizungumza kupitia kipindi cha KatiKati ya Koko, Luiza amesema kuwa si kila rafiki anastahili kupewa nafasi ya kujua kila undani wa maisha yako.
“Siyo kila rafiki ni wa kumweleza kila jambo linalokuhusu. Kuna siku atakushangaza kwa jambo la ajabu litakalokuumiza,” amesema Luiza kwa msisitizo.
Ameeleza kuwa uzoefu wake binafsi umemfundisha kuwa si kila uaminifu hulipwa kwa uaminifu, hivyo ni busara kuweka mipaka hata kwenye urafiki wa karibu.
Ujumbe wake unakuja kama onyo kwa watu hasa vijana, kuwa makini na namna wanavyoshiriki maisha yao ya ndani na wengine, ili kuepuka maumivu yasiyo ya lazima yanayotokana na usaliti au matumizi mabaya ya taarifa binafsi.