Wasomaji waliokutwa maeneo ya Stendi ya Daladala ya Chamazi wakichangamkia kununua magazeti kwa muuzaji wa Global, (mwenye fulana nyeupe kushoto).
Msomaji wa Gazeti la Championi, Selemani Alifa (kulia) wa eneo la Chamazi akimwonesha Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda jinsi alivyojaza kuponi yake.
Rehema Said (kulia), mkazi wa maeneo ya Mbande akijaza kuponi ili kuingia katika droo ya Shinda Nyumba.
Wakazi wa eneo la Chamazi wakizidi kujaza kuponi zao ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
Ibrahim Jumanne (kushoto) akijaza kuponi yake kushiriki bahati nasibu hiyo. Anayeshuhudia kulia ni Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.
Magazeti yakichangamkiwa kununuliwa.
Mkanda (kulia) akimsaidia mmoja wa washiriki wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba kumuelekeza namna ya kujaza kuponi yake.
Wakazi wa Chamazi wakiendelea kujaza kuponi zao.
Mshiriki wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, Said Bia (kulia) akivalishwa kofia na Ofisa Masoko wa Global baada ya kujaza kuponi yake na kushiriki.
Mdau wa Gazeti la Championi, Neema Steven akijaza kuponi yake ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
PROMOSHENI ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd inazidi kuwa kivutio baada ya jana wakazi wa maeneo ya Chamazi, Mbande na Majimatitu, Mbagala  jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kujaza kuponi na kushiriki bahati nasibu hiyo.
Wakazi wa maeneo hayo walionekana kuvutiwa na bahati nasibu hiyo baada ya kukutwa wakinunua magazeti ya Global na kushiriki huku wengi wao wakionesha kiu ya kushinda nyumba ya kisasa katika droo ya mwisho inayotarajiwa kuchezeshwa Juni, mwaka huu.
Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema wanachotakiwa wananchi ni kununua magazeti ya Global na kujaza kuponi zinazopatikana katika magazeti hayo ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Amani, Ijumaa na Risasi Jumamosi ambayo huuzwa kwa shilingi 500, ambapo msomaji yeyote anaweza kujishindia zawadi hiyo kubwa ya nyumba.
Picha/Habari: Denis Mtima, GPL