

Manchester United wameibuka kidedea kwa kuichapa Arsenal mabao 3-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England iliyopigwa Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya Man U yamefungwa na Marcus Rashford aliyetupia mawili na Ander Herrera huku
Danny Welbeck na Mesut Ozil wakifunga mabao ya Arsenal.