ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Yaani hawa walitakiwa kuweka Bajaj kabisa, hata kwa mia mia. Ni mbali sana chooni,” alisema Neema akiwa anakaa.
“Do! Ngoja na mimi niende niuone hata huo umbali,” alisema Bony akisimama kwenda chooni…
“Na mimi, ngoja tuongozane wote shemeji,” alisema Aisha huku akisimama.
JIACHIE MWENYEWE…
Neema wala hakuonesha kushangaa kwa kitendo cha mumewe kwenda chooni na Aisha kutaka waongozane…
“Nendeni mniondolee kiwingu hapa,” alisema Neema akiwa anakatakata maneno…
“Na haturudi tena, utajiju,” alisema Aisha, Neema akacheka sana.
Bony na Aisha waliongozana kwenda chooni maana vyoo vyote vilikuwa eneo moja.
Bony aliingia choo cha kiume na Aisha aliingia kinachomhusu huku akimwambia Bony…
“Shem ukianza kutoka wewe nisubiri tuongozane.”
“Poa…poa.”
Na kweli bwana, Bony ndiye aliyeanza kutoka, akasimama kwenye masinki ya kunawa mikono akimsubiri Aisha. Mara, naye akatoka…
“Twende shem,” alisema Aisha huku akipitisha mkono wake mmoja katikati ya kiuno cha shemeji yake na kuanza kutembea lakini Bony kwa kitendo hicho alishindwa kuvumilia kutoka nje, akasimama…
“Shem,” aliita…
“Bee.”
“Mmm…mwaaa!” Bony alimbusu Aisha…
“Mmm…waaa!” Aisha alijirudishia kisha akaurefusha ulimi wake na kumfanya Bony aupokee kwa shauku, wakazama kwenye denda kwa muda…
“Jamani, kwa nini msiende gesti?” mteja mmoja mwanamke alisema akiwa anaingia chooni na kuwakuta wawili hao wakiwa wamebanana vilivyo.
Aisha alijipangua haraka sana kwa aibu na kuanza kutoka huku mteja huyo akiwaangalia kwani kumbukumbu zake zilimrudisha kwenye meza na kukumbuka kuwa, wawili hao wamekaa meza moja na mwanamke mwingine ambaye ni Neema. Lakini hakujua nani ni mke wa Bony lakini akapata picha kichwani mwake…
“Huyu inawezekana si mkewe. Kama angekuwa mke wake wasingekuja kufanya ujinga huku chooni. Si ajabu mkewe ni yule aliyekaa kule,” alisema moyoni yule mteja akiwa ameshaingia chooni.
Aisha na Bony walirudi sambamba hadi mezani, wakakaa hapo…
“Si mlisema hamrudi tena, imekuaje sasa?” alisema Neema akirudisha mezani glasi yenye pombe baada ya kukata funda moja…
“Tumekuonea huruma peke yako,” alisema Aisha…
“Tumekushtukia pengine una mipango ya kunichepuka,” alidakia Bony, wakacheka.
Yule mteja aliyewashauri kwenda gesti, kumbe alikaa meza jirani na akina Bony. Naye alikaa na mtu wake. Wakati anarudi Aisha alijisikia aibu walipokutana macho…
“Mh! Liangalie kwanza…demu mzuri hata aibu hana. Anakubali kutoa denda chooni, watu wengine bwana, bure kabisa,” alisema moyoni yule mteja akiwa anakaa na akamsimulia jamaa yake…
“Baby, unawaona wale watu pale…yule dada mwenye nguo nyekundu na yule jamaa…”
“Eee…unawafahamu?”
“Noo! Si nimewakuta chooni wanakula denda.”
“Chooni?”
“Ee! Chooni…”
“Mh! Mbona kama hawafanani na kufanya hivyo?”
“Ndiyo ujue sasa wameweza kufanya, mimi nikawaambia jamani si mwende gesti, wakashtuka, wakatoka,” alisema yule mteja mwanamke.
Bony alijua wawili hao wanawazungumzia wao na ni yeye na Aisha, akamtumia meseji Aisha palepale…
“Shem, mbona wale watu kulia kwako wanatuangalia sana, ni ile ishu ya toileti nini?”
Aisha alisikia mlio wa meseji kwenye simu iliyokuwa mkobani na akahisi imetumwa na Bony, kwa hiyo akachukua muda kuchukua simu na kuisoma meseji hiyo.
Baadaye alipoisoma, akaijibu kisha akarudisha simu kwenye mkoba…
“Lazima ni sisi. Noma sana baby! Tusirudie siku nyingine.”
Kwa Neema, pombe kwake zilikuwa zikimpa usingizi mzito. Kulala kwake ilikuwa ni dalili ya kuzidiwa na pombe kwa kiwango cha juu sana. Hivyo, hapo baa alilala, tena kama yupo nyumbani kwake…
“Shem, naona mwenzangu yuko hoi, tuondoke,” alisema Bony akiwa analipa bili ya huduma na dalili zote za kusimama. Aisha naye alisimama, akamshika mkono Neema…
“Mwenzangu tuondoke,” alisema Aisha.
Neema aliamka kwa tabu sana, akashikwa mkono na Bony. Kwa hiyo akawa ameshikwa mikono yote, mmoja Aisha, mmoja Bony.
Kufika nyumbani, Neema aliingia chumbani kwake moja kwa moja na kujitupa kitandani…
“Kwa ninavyomjua, yule hawezi kuamka tena mpaka asubuhi,” alisema Bony naye akienda chumbani, Aisha akamshika mkono…
“Please! Kama kweli hawezi kuamka tena, twende na mimi chumbani kwangu,” alisema…
Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma chombezo hili jipya kwenye Gazeti la Ijumaa, Ijumaa ijayo.