×

Chongo! 26

ILIPOISHIA

Mwani alikuwa kwenye korongo lililo umbali wa kutupa jiwe kutoka nyumbani kwao, eneo ambalo kwa zaidi ya miaka kumi hakuwahi kufika. Akiwa amevaa kaptura ya Jeans nyeusi na kitop cheusi pia, alienda na kukaa chini ya mti ambao chemba iliyotoka kwenye nyumba ya akina Jerry inatokea.

Baada ya kujihakikishia usalama wa kutosha, akainuka na kuanza kuichunguza vizuri chemba..

Sasa endelea…

Tofauti na taarifa za mahusiano ya mastaa kadhaa hivi karibuni, hii ni taarifa ya ‘surprise’ kidogo baina ya wawili hawa, ambapo inasemekana wamea

Ilionekana kama haijafunguliwa kwa muda mrefu na kilichomfurahisha, haikuonyesha kupitisha maji mara kwa mara, kitu kilichompa uhakika kuwa safari ya kutembea kuelekea ndani ya nyumba ingekuwa rahisi.

Ghafla, hisia zikamwonyesha kama kulikuwa na mtu eneo hilo, ingawa ilikuwa ni mchana, mapigo ya moyo wake yakapata mshtuko mkubwa, alipoinua kichwa na kuangalia macho yake yakakutana ana kwa ana na mtu anayemfahamu. Sule!

Alipatwa na mshtuko mkubwa sana, kwa sababu Sule alikuwa mmoja wa watu waliotakiwa na akina Bata, hivyo kuonekana kwake katika eneo lile muhimu sana kwao, lilimpa mashaka makubwa. Uzoefu wa kikachero wa Sule, ulisoma kitu kutokana na mshtuko huo, lakini hakutaka kuonyesha.

“Mambo baby? Nimekuona wakati unazunguka pale nyuma kwenu, nikasema nije nikusalimie,” Sule alimwambia Mwani, ambaye sasa alishusha pumzi na kuona uhuru wa nafsi yake ukirejea. Akaachia tabasamu pana lililomfariji sana kijana huyo mwenye mwili mkakamavu.

Kwa mara ya kwanza katika harakati zake, aligundua kuwa anaweza kushinda vita vya kumtafuta binti huyo baada ya kushindwa mara nyingi.

Na bila kutarajia, Mwani akajisikia mtu mwenye bahati sana kukutana na Sule maeneo yale, kwani aliamini angeweza kupata kitu cha kuwasaidia. Akili yake iliamua kumsaidia Bata kwa kadiri atakavyoweza.

“Poa tu Sule, vipi za siku?,” alisema Mwani, ambaye hapo awali kabla hajatongozwa, alikuwa akimwamkia Sule, kwani alimzidi sana umri.

“Aah, mimi bado nataabika tu na penzi lako, sijui wewe mtoto nilikukosea nini ambacho huwezi kunisamehe. Hivi hujui kama hata mimi ukinitoboa natoka damu?” Sule alianza kuimbisha kwa mara nyingine.

“Nani asiyewajua nyinyi wanaume, mkikubaliwa mara moja hamkawii kusema ‘maharage ya Mbeya yule’, mkibaniwa hamuishi kulalamika, bwana wakati mwingine mtu unaona bora lawama,” alisema Mwani, akiwa na tabasamu lililompa sana matumaini Sule.

“Sasa hivi wewe unafikiri kwa muda wote huo mimi naweza kukuita maharage ya Mbeya kweli? Sijawahi msotea binti kama ilivyo kwako. Sasa sikia nikuambie kitu, hebu saa kumi tukutane basi Coco, n’takuwa ile baa ya kitimoto,” Sule alichombeza!

Hakuwahi kuamini kama ingekuwa rahisi kiasi hicho, alijiona mtu mwenye bahati kwa sababu hata kuonana kwenyewe siku hiyo kulikuwa kwa bahati. Kwa mara ya kwanza Mwani akakubali kuchukua namba ya simu ya Sule na kumpa yake. Wakati wakiagana, Sule alimpatia shilingi laki moja ya kupandia teksi.

***

Alipofika nyumbani kwao, Mwani alimpigia simu Bata na kumweleza kila hatua aliyopiga. Baada ya kubadilishana maneno mawili matatu, wakakubaliana kwamba ni vizuri na akina Bata nao wakawepo eneo la tukio, ili kumfahamu Sule.

Sule akatumia muda huo kumpigia simu Elina na Juddy na kuwafahamisha kuhusu maendeleo ya ishu yao. Nao wakaafiki wazo la kuwepo Coco, hivyo harakaharaka walifanya maandalizi na ilipofika saa tisa na robo, vijana hao watatu walikuwa wamekaa kwenye meza iliyo pembeni kabisa, wakiitazama Bahari ya Hindi kwa ukaribu.

Ni muda huo ndipo Sule alipompigia simu Mwani na kumweleza kuwa alikuwa njiani kuelekea sehemu ya miadi na kumkumbusha kuzingatia muda, jambo ambalo msichana huyo alilikubali kana kwamba ni wapenzi wa muda mrefu.

Akiwa katika mavazi ambayo mwanaume yeyote asingekubali kumuachia kwa macho bila kumpa neno, Mwani aliondoka nyumbani kwao saa kumi na dakika tano na alipotokea tu barabarani, aliipungia mkono Bajaj iliyokuwa ikipita kwa mwendo wa kasi.

“Coco mara moja kaka,” alimwambia dereva huku akiwa anaingia bila hata kuelewana bei.

“Buku tano tu sista,” alisema dereva huyo. Mwani hata hakusema kitu, alifungua pochi ndogo iliyokuwa ndani ya mfuko wa suruali yake ya jinzi aliyovaa na kumpatia shilingi elfu kumi.

 Mwani alikuwa mzoefu sana wa maeneo ya Coco, maana kila wikiendi ilikuwa ni lazima aende, hivyo alimuelekeza dereva sehemu ya kushuka, mbali kidogo na baa aliyoelekezwa, halafu akaanza kutembea taratibu kwa madoido.

Katika watu waliokuwa ndani ya baa hiyo, akina Bata hawakuweza hata kumhisi kijana anayemsubiri Sule na walipomuona Mwani akija kwa madaha, wakajifanya kutokuwa na habari naye.

Itaendelea wiki ijayo

Leave a Comment